Zahera alisaini mkataba wa miaka miwili kuifundisha timu hiyo yenye maskani yake ya Twiga na Jangawani.
Akizungumza na Mwanaspoti, alisema ameona habari nyingi zikienea kwamba ameshindwa kurejea nchini kutokana na kudai malimbikizo ya mshahara katika kikosi cha Yanga.
"Ningekuwa sirudi basi mimi mwenyewe ningesema, maisha yangu yapo hata nje ya mpira na sio kwamba mpira ndio unanipa namna ya kuishi, nina watu 42 Congo na watu wanne Ulaya, hivyo naweza kufundisha timu yoyote hata kwa miaka mitatu bila kulipwa," alisema.
Aliongeza alifika Ufaransa tarehe 13 na alipanga kupumzika kwa siku 15 kutokana na kutopata muda wa kupumzika wa kutosha.
"Narudi hivi karibuni tu, mtashtuka nipo hapo lakini sikupata muda wa kupumzika kutokana na Ligi na mechi za mfululizo," alisema.
No comments:
Post a Comment