Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amepokea masanduku mawili ya dhahabu yenye uzito wa kilo 35.34, pamoja na fedha, yakitokea Kenya kufuatia kukamatwa na vyombo vya ulinzi vya nchi hiyo.
Akizungumza wakati akipokea dhahabu na fedha hizo, Rais Magufuli amewataka Watanzania kumpongeza yeye na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta kwa kuwa waaminifu, kwa kuwezesha fedha na dhahabu hizo kurejeshwa Tanzania.
Magufuli amesema kuwa "vitu vya fedha na dhahabu vinahitaji moyo wa jiwe, kiukweli Rais Kenyatta ni muaminifu, zingeweza kupigwa juu kwa juu, lakini fedha hizi zimerudi Tanzania baada ya miaka 15. Na mimi mnipongeze pia inawezekana wangekuwa wengine wangepiga dili juu kwa juu, na wala msingejua."
Aidha Rais Magufuli amesema kuwa "wakupongezwa kwa hili ni vyombo vya Kenya, najua wakuu wa vyombo vya ulinzi Tanzania mpo hapa, lazima niwatandike kwa sababu vitu vimetoka Mwanza vimekamatiwa Kenya, je zilipobebwa Mwanza na Kilimanjaro, vyombo vyetu vilikuwa vinafanya nini? amesema Rais Magufuli.
Awali Waziri wa Mambo ya Nje Mh. Palamagamba Kabudi, amesema nchi hizo mbili zimekuwa na uhusiano wa muda mrefu, hasa kwenye masuala ya uchumi na siasa.
"TANU na KANU zilikuwa ndugu, TANU ilipeleka watu Kenya kufanya siasa, hata Land Rover ya kwanza iliyotumiwa na Katibu Mwenezi wa KANU, ilitoka TANU ili kumpigania Jomo Kenyatta, pamoja na Kenya ipate uhuru kwa hiyo mahusiano ni ya undugu." amesema Kabudi.
No comments:
Post a Comment