Beki Kelvin Yondani na mlinda lango Aishi Manula juzi jioni walishindwa kufanya mazoezi na kikosi cha Stars kinachojiandaa na mchezo dhidi ya Algeria utakaopigwa leo Jumatatu dimba la Al Salaam
Wachezaji hao walipata majeraha kwenye mchezo dhidi ya Harambee Stars uliomalizika kwa Tanzania kulala kwa mabao 3-2
Licha ya sintofahamu hiyo, Daktari wa Stars Richard Yomba amesema wachezaji hao wanaweza kucheza mechi ya leo
Yomba amesema waliwapa mapumziko juzi ili waweze kupona majeraha madogo waliyopata kwenye mchezo dhidi ya Kenya
Kuelekea mchezo huo Stars tayari imewapoteza Erasto Nyoni aliyeumia na Mudathir Yahya mwenye kadi mbili za njano
Aidha Farid Mussa na David Mwantika nao wameonekana kutokuwa 'fit' licha ya kuendelea na mazoezi
Yomba amesema wachezaji hao hawana majeraha makubwa hivyo wanapatiwa tiba maalum
Stars itachuana na Algeria leo katika mchezo ambao matokeo ya ushindi yanaweza kuipeleka Stars hatua ya mtoano lakini matumaini hayo madogo yatategemea na matokeo ya timu nyingine
No comments:
Post a Comment