Klabu ya soka ya Yanga imewapiku mahasimu wao wa jadi Simba katika kutambulisha wimbo rasmi wa klabu kuelekea msimu mpya wa Ligi Kuu na michuano ya Kimataifa.
Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Yanga imetambulisha wimbo wake rasmi utakaotumiwa katika michuano mbalimbali kuanzia msimu huu, na kusisitiza kuwa ni wajibu wa wanachama na mashabiki kuufahamu wimbo huo.
Kama tulivyoahidi kwamba katika #WikiYaMwananchi tutatambulisha wimbo rasmi wa #YangaSc (Club Anthem) tunayo furaha kuuleta kwenu wimbo huu.
Kazi ni kwako, hakikisha unaufahamu vizuri wimbo uje kuimba na wananchi katika siku ya mwananchi.#ImbaNaWananchiSikuYaMwananchi
15 people are talking about this
Wimbo huo wa Yanga utaanza kutumika katika mchezo wao wa Kimataifa wa 'Wiki ya Wananchi', Agosti 4 dhidi ya Kariobangi Sharks ya Kenya.
Mahasimu wao Simba waliahidi kutoa wimbo wao rasmi wa klabu ifikapo Agosti 3, 2019, wimbo ambao utaanza kutumika katika mchezo wao wa Kimataifa wa Simba Day, Agosti 6 dhidi ya Power Dynamo ya Zambia.
No comments:
Post a Comment