Kiungo aliyewahi kutamba nchini Jerry Santo ambaye sasa anacheza ligi kuu ya Kenya timu ya Posta, amesema uongozi wa Yanga umefanya uamuzi sahihi kumsajili mlinda lango Farouq Shikalo
Shikalo ametua Yanga kwa mkataba wa miaka miwili akitokea klabu ya Bandari Fc ya Kenya
Mlinda lango huyo mahiri alikuwemo kwenye kikosi cha Harambee Stars kilichoshiriki fainali za Afcon 2019 na kuondoshwa hatua ya makundi
Santo amesema mapungufu yote ambayo msimu uliopita yalijitokeza katika eneo la kipa hasa baada ya kuondoka kwa Beno Kakolanya, sasa wameyapatia ufumbuzi na anawapongeza kwa kufanikisha usajili huo.
"Yanga wamepata bonge la kipa, Shikalo ni kipa bora kabisa hapa Kenya kwani amekuwa akifanya vizuri sana na ninaamini atakuwa msaada mkubwa kwa Yanga," amesema
"Shikalo namjua vizuri sana, Yanga wamepata kipa mzuri, wapinzani wajipange tu kuiona kazi yake uwanjani"
Usajili wa Shikalo umefanikishwa kwa kiasi kikubwa na kocha Mwinyi Zahera ambaye mwenyewe alichukua jukumu la kufanya nae mazungumzo baada ya hapo mwanzo viongozi wa Kamati ya usajili kumuangusha wakati wa usajili wa dirisha dogo
Shikalo anatarajiwa kuwa kipa namba moja wa Yanga

No comments:
Post a Comment