Baada ya kuenea kwa taarifa kuwa uongozi wa timu ya As Vital umesema hawatokuja nchini Tanzania kucheza mchezo wa kirafiki na Yanga kwasababu ya kubadilika kwa ratiba ya michezo ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Africa, timu ya Yanga imesema bado wanajiandaa na mtanange huo.
Dar24 imefanya na mahojiano ya moja kwa moja na afisa habari wa klabu ya Yanga, Dismas Ten amesema hawajapokea barua kutoka kwa As Vital kuhusiana na timu hiyo kutokuja nchini kwaajili ya kushiriki mchezo huo ambao unatarajiwa kuchezwa Agost nne mwaka huu katika kilele cha wiki ya mwananchi.
Ten amesema bado wapo kwemye maandalili ya mchezo huo kwani hawana taarifa ya aina yoyote wala hawajapokea barua kwamba timu hiyo haitokuja nchini kutokana na kubanwa na ratiba za CAF kwaajili ya michezo ya awali ya ligi ya mabingwa barani Africa ikionesha mchezo wa kwanza wataanzia ugenini dhidi ya USM de Loum ya nchini Cameroon Agosti 9 hadi 11 mwaka huu.
As Vital walikubali mwaliko huo kwasababu ratiba ilionesha wataanzia hatua ya 32 bora ila kutokana na mabadiliko hayo huenda ikawalazimu kubadili mipango yao ambayo waliiweka hapo awali
No comments:
Post a Comment