Msanii wa kiume kutoka kiwanda cha Bongo Movie hapa nchini Tanzania Yusuph Mlela, amenyoosha maelezo kwa kile kinachodaiwa wasanii wengi wa BongoMovie ni wadananda.
Msanii huyo amefunguka hayo kupitia EATV & EA Radio Digital, baada ya kuulizwa kuhusu maisha ya wasanii wa Bongo Movie kuwa wadananda na kutegemea maisha ya watu wengine kuanzia kula kuvaa hadi makazi.
"Hapana sio kweli, mtu kama unajitambua hauwezi kuwa mdananda, mimi ninaishi maisha simtegemei mtu yeyote, labda kila mtu ana uonevu wake na jinsi mtu anavyofikiria na labda yeye kaona hivyo lakini mimi maisha yangu simtegemei mtu".
Aidha msanii huyo ameendelea kueleza kuhusu suala la wasanii wengi wa Bongo Fleva kama Quick Rocka, Nandy na Lulu Diva kuvamia upande wa Bongo Movie.
"Sio mbaya kwa sababu sanaa ya BongoMovie bado ni changa na ndogo, hivyo wanahitaji watu wengi zaidi wenye vipaji ili kuzidi kutanua wigo na wataendelea kuwapokea na kuwaunga mkono wasanii wa BongoFleva wanaofanya filamu kwa sasa" amesema Yusuph Mlela.
No comments:
Post a Comment