Leo Julai 23, 2019 Uingereza imepata Waziri Mkuu mpya, Boris Jonson atakayechukua nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa waziri mkuu wa taifa hilo, Bi. Theresa May.
Boris Johnson amemshinda mshindani wake ndani ya chama cha Conservative, Jeremy Hunt kwa kura 92,157 kwa 46,656.
Boris alishawahi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza kuanzia mwaka 2016 hadi 9 Julai 2018 .
Kabla ya zoezi la kumpata Waziri huyo,Takribani Mawaziri 14 nchini Uingereza walitangaza kujiuzulu nafasi zao, kwa kile walichokidai kupinga utawala wa Boris Johnson, ambaye alionekana kupewa nafasi kubwa kushinda uchaguzi huo.
Johnson ameahidi kufanya mageuzi makubwa hususani kuangalia upya muswada wa mkataba wa Brexit uliomtoa madarakani Bi. Theresa May.
No comments:
Post a Comment