Kwa mara ya kwanza tangu kusambaa kwa taarifa zinazodaiwa kwamba ni mpasuko ndani ya chama cha mapinduzi CCM ikiwemo kusambaa kwa sauti zinazodaiwa kuwa ni za baadhi ya wanachama na viongozi wa chama hicho, leo July 23, 2019 Katibu mkuu wa CCM Dr. Bashiru Ally ametoa kauli yake katika mkutano na wajumbe wa chama hicho uliofanyika mkoani Dodoma.
“Wapuuzeni hao wapumbavu, wapuuzeni kabisaaa na ole wake mwanaCCM abainike anafanya malumbano ya kilejaleja tutachukua hatua, maana kuna watu hapa wanaweza wakataka watumie upuuzi unaoendelea kujifanya wao ndio makada na kutafuta kiki, utafukuzwa kwasababu tunazo kanuni zetu”-Dr. Bashiru Ally
No comments:
Post a Comment