Uongozi wa Yanga umesema timu itacheza michezo minne ya kujipima kabla ya kurejea jijini Dar es salaam kuhitimisha wiki ya Mwananchi ambayo tarehe yakeitatangazwa baadae
Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga Dismas Ten amesema michezo hiyo itapigwa mkoani Morogoro na Dodoma
Mchezo wa mkoani Dodoma ni dhidi ya Dodoma Fc ambao utapigwa Julai 23
Michezo mingine itapigwa Julai 15, 19 na August 03
Ten amesema wataitumia michezo hiyo kuwapa fursa wakazi wa mikoa ya Morogoro, Dodoma na maeneo ya jirani kukishuhudia kikosi chao kipya
Amewataka mashabiki wasipoteze fursa hiyo kwa kujitokeza kwa wingi uwanjani kuiona timu yao
Yanga inaendelea kujifua mkoani Morogoro

No comments:
Post a Comment