Mwili wa mtu umepatikana nyumbani kwa kiungo wa kati wa Arsenal Mohamed Elneny nchini Misri.
Babake Elneny, Nasser aliupata mwili huo wakati alipotembelea nyumba hiyo mjini Mahalla al-Kubra , ambayo iko takriban kilomita 100 kaskazini mwa Cairo.
Kwa mujibu wa BBC. Kisa hicho kiliripotiwa kwa polisi, ambaye wanasema mtu huyo alikuwa akijaribu kuiba nyaya za umeme.
Inaaminika kwamba alichomwa na umeme wakati wa wizi huo. Nyumba hiyo ni mali mpya ambayo ilitolewa na familia ya Elneny kutumika kama ofisi.
Elneny ambaye amerudi Arsenal baada ya kuichezea Misri katika kombe la mataifa ya Afcon , aliambiwa kuhusu kisa hicho kupitia simu.
No comments:
Post a Comment