Waziri wa Fedha nchini Kenya, Henry Rotich, amejisalimisha kwa maofisa wa upelelezi leo, muda mfupi baada ya mkurugenzi wa mashtaka nchini humo kuagizwa akamatwe.
Kwa mujibu wa shirika la Nairobi News, Rotich alipelekwa kwa gari hadi katika makao makuu ya idara ya upelelezi ambako anahojiwa kuhusu malipo yaliyotolewa kwa ujenzi wa mabwawa mawili nchini.
Anatuhumiwa kukiuka muongozo wa utoaji wa kandarasi iliyopewa kampuni ya Italia iitwayoCMC de Ravenna yenye thamani ya zaidi ya dola milioni 450 kwa ujenzi wa mabwawa. Hapo awali, mkurugenzi wa mashtaka, Noordin Haji, aliagiza kukamatwa kwa Rotich ili ashtakiwe kwa ufisadi
Mkurugenzi huyo wa mashtaka amekuwa akizungumza katika vyombo vya habari kuhusu uamuzi wa kumshtaki Rotich, na maofisa wengine wa serikali kuhusu kandarasi zilizotolewa kwa kampuni hiyoya Italia ili kujenga mabwawa mawili.
Haji ameeleza kwamba watashtakiwa kwa “kupanga kufanya udanganyifu, kushindwa kutii muongozo unaotumika katika upatikanaji wa kandarasi” miongoni mwa mambo mengine. Mashtaka hayo yanahusiana na ujenzi wa mabwawa mawili nchini uliogharimu fedha nyingi.
Mnamo Rotich alikana, kupitia tangazo kubwa kwenye gazeti nchini humo, kwamba alifanya makosa yoyote. Pia, kampuni hiyo ya Italia tuhuma hizo
No comments:
Post a Comment