Waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi Kangi Lugola ameliagiza Jeshi la Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Ilala jijini DSM Kufanya Operesheni Maalum ya usiku na mchana ya kuwasaka na kuwakamata Vibaka na waporaji ambao wamekuwa wakiendesha vitendo vya uhalifu vya wizi na uporaji katika eneo la Jangwani hasa nyakati za jioni na usiku.
Waziri Ligola ametoa agizo hilo kwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa kipolisi wa Ilala wakati alipofanya ziara ya ghafla katika eneo la Jangwani eneo la Club ya Yanga ambako vibaka na waporaji wameweka makazi maalum na kuendesha uhalifu na kujificha katika eneo hilo.
No comments:
Post a Comment