Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. John Pombe Magufuli leo amemuapisha George Boniface Simbachawene kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira na Hussein Mohamed Bashekuwa Naibu Waziri wa Kilimo.
Hafla ya kuapishwa kwa viongozi hao imefanyika Ikulu Jijini DSM na kuhudhuriwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Jaji Mkuu wa Tanzania Prof. Ibrahim Hamis Juma,Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, Mawaziri, Naibu Mawaziri, Makatibu Wakuu na Viongozi Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama.
Rais Magufuli amewapongeza viongozi hao kwa uteuzi walioupata na amewataka kwenda kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi na kurekebisha kasoro zilizopo katika wizara zao ili kuleta matokeo yanayotarajiwa.
No comments:
Post a Comment