We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Monday, July 22, 2019

Kigwangalla amwambia jambo Waziri Mkuu

Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamis Kigwangalla, amemhakikishia Waziri Mkuu na wananchi wa eneo la Ngorongoro kwamba, Wizara iko katika mchakato wa kuhakikisha ushirikiano na uhusiano mzuri unakuwepo kati ya wananchi na wahifadhi, katika Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro.

Waziri Kigwangalla ameyabainisha hayo leo Julai 22, wakati akijibu changamoto iliyobainishwa na Waziri wa Elimu William Ole Nasha, juu ya migogoro iliyodumu kwa takribani miaka 60 sasa, iliyopo kati ya wananchi wanaoishi ndani ya hifadhi hiyo na wahifadhi.
Ambapo amesema, Wizara imefanya utafiti mkubwa na wa kisayansi,  kuhusu hatma ya uhifadhi na maisha ya watu wa Ngorongoro.
''Kumekuwa na migongano inayojitokeza na ambayo iko wazi, wakati hifadhi inatangazwa wananchi  wa hapa, Mh Waziri Mkuu, walikuwa elfu 8 lakini leo wako laki moja,  na sasa kuna jumla ya asilimia 25 ya wakazi wa hapa hawana Ng'ombe, mbuzi, kuku wala kondoo, kwahiyo ni lazima sasa wanahitaji kula tofauti na zamani na mahitaji pia yameongezeka'', amesema Dkt Kigwangalla.
Aidha Kigwangalla ameongeza kuwa ili kuweka usawa wa hayo yote ni vigumu na ni lazima migogoro itarajiwe sababu idadi ya watu imekuwa kubwa, mifugo ni mingi hivyo kuna haja ya kutafuta suluhisho la kudumu.
Waziri wa Elimu William Ole Nasha aliomba, ipatikane suluhu kudumu  kati ya wahifadhi na wananchi wa Ngorongoro na kudai kwamba hali ya sasa imekuwa tofauti na awali ambapo wavumbuzi wa fuvu la binadamu wa kale, Dr Leakey na mkewe walikuwa wakiishi vizuri na wakazi wa eneo hilo.

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list