We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Monday, July 22, 2019

BAKWATA Dodoma Waazimia Kutofanya Kazi Na Mkurugenzi Wa Uchumi,Mipango na Uwezeshaji

Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
MKUTANO mkuu wa Baraza la Waislamu Mkoa wa Dodoma (BAKWATA) umeazimia kutofanya kazi na Mkurugenzi wa Uchumi,Mipango na Uwezeshaji Ustadh  Othmani Shabani Hotty kutokana na kile kilichodaiwa kutotambua nafasi aliyochaguliwa kwenye mkutano mkuu wa vijana jumuiya ya vijana BAKWATA taifa (JVBT) .

Maazimio hayo yamepitishwa kwenye kikao cha mkutano huo mbele ya Shekhe wa mkoa wa Dodoma Mustafa Rajabu na wajumbe kutoka Bakwata taifa kilichokaa kwa ajili ya kupokea taarifa za kimaendeleo kutoka wilaya zote,za Mkoa wa Dodoma na ikiwemo na changamoto zinazolikabili Baraza hilo la Bakwata Mkoa.

Katika kikao hicho kilichowakutanisha mashehe,wenyeviti na makatibu wa baraza la BAKWATA,kwa pamoja lilisema kuwa katika uteuzi wake hawakutarifiwa kama baraza juu kuhusu nafasi aliyoteuliwa ya Ukurugenzi wa uchumi na uwezeshaji.

 yapo mambo ambayo yamekuwa yakiendelea katika kukwamisha Bakwata kutokana na kuwepo kwa baadhi ya watu wanaokuwa viongozi lakini wamekuwa wakifitinisha waislamu na viongozi kwa lengo la kutengeneza Migogoro.

Katika kikao hicho ambacho pia kiliudhuriwa na viongozi kutoka BAKWATA,Taifa baadhi ya wajumbe,walisema kuwa Baraza la BAKWATA Mkoa wa Dodoma haliwezi kufanya kazi na watu ambao wamekuwa wakifitinisha waislamu wenzake.

Kwenye kikao hicho ambacho kilikuwa kikiongozwa na Sheik wa Mkoa wa Dodoma Alhaji Mustafa Rajabu,alisema Bakwata mkoa wa Dodoma umekuwa na baadhi ya watu ambao wamekuwa wakifanya fitina kwa kutengeneza majungu kwa misingi ya kutaka Baraza kuyumba.

Wajumbe hao walisema kuwa uongozi wa Mkoa hauwezi kukubaliana na uteuzi wa Othumani Hotty kuwa uteuzi uliofanyika haukushirikisha uongozi wa Mkoa.

Uongozi huo ulitakiwa kufanya uteuzi kwa kumshirikisha katibu Mkuu wa Bakwata na kwa utaratibu ilifaa jina la uteuzi lianzie ngazi ya Wilaya mkoa na ndo jina lipelekwe makao makuu.

Aidha Sheik Alhaji Mustafa alisema kuwa yapo mambo mangine ambayo yaliaribika kutokana na kuwepo kwa watu waliokuwa wakifanya kazi kwa kujinufaisha mwenyewe na kusababisha kuwepo kwa tabia ya kubinafsisha mali ya BAKWATA.

Akizungumzia mafanikio ambayo Sheikh Alhaji Mustafa katika uongozi wake pamoja na viongozi ni pamoja na  Kuinusuru shule ya sekondari ya Hijila pamoja na viwanja vyake.

Alisema kuwa kutokana na kuwepo kwa uongozi uliokuwepo kwa kipindi ambacho alitengenezewa majungu na fiti wale waliokaimu walitumia nafasi hiyo kujinufaisha pamoja na kusababisha ubadhirifu mkubwa wa mali za Bakwata Mkoa wa Dodoma na kutengeneza migogoro.

katika hatua nyingine wajumbe kutoka mikoani kutoka wilayani walisema kuwa kwa kipindi ambacho sheiki wa Mkoa kusimamishwa viongozi waliokaimishwa uongozi walikuwa wakiwadharau viongozi kutoka wilayani kutokana na kupuuzwa jambo ambalo lilisababisha kushindwa taarifa ambazo zipo katika maadishi kutofika ofisini.

Hata hivyo wajumbe hao wameazimia katika kikao hicho wamesema kuwa umefika wakati wa kuwachukulia hatua waumini wa dini ya kiislamu ambao wamekuwa wakikwamisha juhudi za kujenga Bakwata pamoja na kutengeneza migogoro ndani ya baraza.

Kwa upande wake Athumani Hotty aliyeazimiwa kutofanya kazi na Mkurugenzi wa Uchumi,Mipango na Uwezeshaji,alisema kuwa kikao hicho hakina uwezo wa kumuazimia kwa kuwa yeye mamlaka yake ni ya kitaifa na siyo ya kimkoa.

Hotty alisema kuwa yeye uteuzi wake ni wamitaifa na ni kwa ngazi ya baraza last vijana kutokana na hali hiyo mamlaka ya kumuazimia yanatoka taifa na baraza la vijana wanautaratibu wake.

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list