WATU 10 wameripotiwa kupoteza maisha katika Jimbo la Texas baada ya kutokea kwa ajali ya ndege binafsi katika eneo la Uwanja wa Ndege katika Manispaa ya Addison nchini Marekani.
Taarifa zinaeleza kuwa, ndege hiyo ilipoteza mwelekeo wakati ikiruka hali iliyosababisha kujibamiza na kuwaka moto.
Watu saba kati ya watu 10 waliuawa katika ajali hiyo walitambuliwa jana Jumatatu huku kifaa cha kurekodi ya sauti ya cockpit kutoka kwenye ndege kikipatikana.
Mpaka sasa mamlaka hazijatoa sababu ya ajali hiyo iliyotokea juzi Jumapili asubuhi.
Kati ya waliofariki, watu 4 ni ndugu wa familia moja.
No comments:
Post a Comment