We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Wednesday, July 31, 2019

Walichokisema Idara ya Uhamiaji kuhusu Mwandishi Erick Kabendera


Kamishna wa Uraia na Pasipoti Uhamiaji, Gerald Kihinga amesema kuwa Mwandishi wa habari, Erick Kabendera aliyedaiwa kutoweka nyumbani kwake idara ya uhamiaji wanae na wanaendelea kumhoji utata wa uraia wake.

Kamishna Kihinga amesema kuwa Uhamiaji walipata taarifa kutoka kwa wasamalia wema kufuatia utata wa uraia bwana Erick Kabendera.

"Uhamiaji tulipata taarifa kutoka kwa wasamalia wema kufuatia utata wa uraia wa bwana Erick Kabendera baada ya idara kupewa tarifa hizo tulianza kuzifanyia kazi hata hivyo Kabendera mwenyewe hajawahi kuhojiwa kulingana na Uraia wake kwakuwa hakufika katika ofisi ya uhamiaji pamoja na kutumiwa wito mara nyingi lakini hakuweza kufika, " amesema Kamishna Kihinga.

"Uhamiaji kushirikiana na jeshi la Polisi tuliweza kumtafuta na kumpata na mpaka tunavyoongea hivi bwana Kabendera tunae sisi uhamiaji kwaajili ya kumhoji kuhusu utata wa uraia wake.

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list