Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Tiba Asilia Taifa (SHIVIWATA), Abdulraman Lutenga, amepiga marufuku waganga wote wa jadi nchini kutoa huduma za tiba katika nyumba za kulala wageni.
Marufuku hiyo imekuja baada ya malalamiko ya muda mrefu ya wateja wanaokwenda kupata huduma katika maeneo hayo, hasa wanawake, kwamba wamekuwa wakifanyiwa na waganga hao vitendo vya udhalilishaji ikiwemo ubakaji.
Akizungumza katika kikao cha pamoja kilicholihusisha Jeshi la Polisi Mkoa wa Iringa na waganga hao kutoka mkoani Irings, Lutenga alisema kuanzia sasa yeyote atakayekutwa anatoa huduma katika nyumba za kulala wageni atachukuliwa hatua kali za kisheria.
Alisema kuwa sheria zao zinamtaka mganga wa tiba asilia kuwa na sehemu yake maalumu ya kufanya kazi hiyo na sio katika nyumba za kulala wageni na barabarani kwani wataalamu wengine ambao si waaminifu hutumia mwanya huo kuwafanyia vitendo viovu wateja wao.
No comments:
Post a Comment