Nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars baada ya kupoteza katika mchezo wao wa mwisho wa Kundi C dhidi ya Algeria kwa magoli 3-0, Mbwana Samatta ameongea na waandishi na kueleza kupokea kwa masikitiko matokeo hayo lakini akieleza hiyo ni kama fursa kwao ya kujua michuano hiyo na kupata uzoefu.
“Ni mashindano makubwa namshukuru Mungu nimeweza kucheza mechi zote nipo salama lakini nadhani nahitajika zaidi kufanya bidii zaidi ya nilizokuwa nazifanya kwa sababu nimeona kuna ugumu wake kucheza na timu kama hizi hapa ambazo zimepiga hatua sana lakini kama timu tuna safari naona”>>>Samatta
“Nashukuru Mungu tumepata nafasi ya kuwa katika mashindano haya ni kitu ambacho kiukweli kimetufundisha kwa kiasi kikubwa safari yetu bado ipo tunahitaji kufanya bidiii, bado kuna safari kuna mlima mkubwa inabidi tuushinde kila eneo, nadhani vitu ni vingi tu maandalizi wachezaji nafikiri wanahitaji kwenda kucheza proffesional wengi sana ili kuweza kuendana na mashindano kama haya”>>>Samatta
Timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars kwa matokeo hayo imeondolewa rasmi kwa kuwa nafasi ya mwisho katika Kundi C ambalo lina timu za Algeria anayeongoza kwa kuwa na point 9, wakifuatiwa na Senegal wenye point 6 na Kenya nafasi ya tatu kwa kuwa na point tatu walizozivuna dhidi ya Tanzania.
No comments:
Post a Comment