Awamu ya kwanza ya dirisha la usajili kwa ajili ya michuano ya Shirikisho la soka barani Afrika (CAF) limefungwa leo
Kulingana na taarifa iliyotolewa na CAF, kuanzia kesho kwa timu zilizochelewa kuwasilisha majina ya vikosi vyao, zitalazimika kulipia dola 500 kwa kila mchezaji
Faini hiyo itaendelea kuongezeka hadi kufikia Julai 31 ambapo timu ambazo zitakuwa hazijawasilisha majina hazitaruhusiwa kushiriki michuano ya msimu ujao
Simba imetuma majina ya wachezaji 25 ikiwa na nafasi tano ambazo wanaweza kuzijaza kati ya sasa na kabla ya kuanza kwa hatua ya makundi

No comments:
Post a Comment