We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Tuesday, July 9, 2019

Umoja wa Afrika kujadili matumizi ya pesa ya pamoja

Viongozi wa nchi za Afrika wamekutana katika mkutano maalumu wa 12 wa nchi za Umoja wa Afrika unaofanyika nchini Niger.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya nchi hiyo, mkutano huo ulianza mjini Niamey chini ya ulinzi mkali.

Viongozi hao wa nchi za Afrika watajadiliana mambo mengi ikiwamo eneo la biashara huru barani Afrika (AfCFTA), matumizi ya pesa ya pamoja, masuala ya usalama, ugaidi na mambo mengineo.

Mwenyeji wa mkutano huo Rais wa Niger, Mahamadou Issoufou, alisema kupita kwa mkataba wa AfCFTA itakuwa ni faida kubwa kwa nchi zote za Afrika.

Umoja wa  Afrika una jumla ya wakazi wapatao bilioni  1,2  na pato ghafi la dola trilioni 2,5.

Mkataba huo ulikubaliwa na nchi zote za Afrika isipokuwa Eritrea. Mkataba wa AfCFTA unaruhusu biashara za ndani ya bara kuwa na punguzo katika kodi ya forodha la asilimia 90. 

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list