Uganda imefanikiwa kutinga hatua ya 16 bora michuano ya Afcon 2019 inayoendelea nchini Misri baada ya kumaliza nafasi ya pili kundi A
Licha ya kufungwa mabao 2-0 na Misri kwenye mchezo wa mwisho, Uganda imefuzu hatua ya mtoano na sasa itachuana na Senegal au Kenya kwenye hatua hiyo
Mabao ya Mohammed Salah na Ahmed Elmohamady yaliizamisha Uganda usiku wa kuamkia kwenye mchezo wa mwisho kundi A dhidi ya wenyeji Misri ambao wamefuzu wakiwa na alama tisa baada ya kushinda michezo yote mitatu
Aidha nayo DR Congo imefufua matumaini ya kutinga hatua ya mtoano kupitia 'best looser' baada ya kuifumua Zimbabwe mabao 4-0
DR Congo imemaliza katika nafasi ya tatu kundi A ikiwa na alama tatu wakati Zimbabwe imeyaaga mashindano hayo ikiwa na alama moja
Katika michezo iliyopigwa mapema jana kundi B, Madagascar iliiduwaza Nigeria kwa kuichapa maao 2-0 hivyo kutinga hatua ya 16 bora ikiwa vinara wa kundi hilo baada ya kufikisha alama saba
Nigeria imemaliza nafasi ya pili ikiwa na alama sita
Guinea nayo inaweza kutinga 16 bora kupitia nafasi ya 'best looser' baada ya kujikusanyia alama nne
Burundi imeyaaga mashindano hayo baada ya kufungwa michezo yote mitatu
Timu hiyo pia haikufunga bao hata moja
No comments:
Post a Comment