Real Madrid wana mpango wa kumjumuisha mshambuliaji wa Wales Gareth Bale, 29, katika mkataba utakaowawezeesha kumnunua kiungo wa kati wa Manchester United na Ufaransa Paul Pogba, 26. (Mail)
United watalazimika kilipa zaidi ya pauni milioni £90 kumnunua beki wa Leicester City na England, Harry Maguire - hatua itakayomfanya kuwa nyota huyo wa miaka 26 kuwa mlizi ghali zaidi . (Telegraph)
United pia imetuma maombi ya kumnasa kiungo wa kati wa Uhispania na Dinamo Zagreb-Dani Olmo, 21. (Mail)
Mshambuliaji wa Arsenal na Ufaransa Alexandre Lacazette, 28, huenda akahama klabu hiyo msimu huu wa joto. (Express)
GETTY IMAGES
Mlinzi wa Bournemouth na Uholanzi Nathan Ake, 24, huenda akatia saini mkataba wa kujiunga na Manchester City mhumu ujao. (L'Equipe, via Manchester Evening News)
Crystal Palace wanafanya kila juhudi kuhakikisha hawataiuzia Arsenal winga wa Ivory Coast Wilfried Zaha, 26, na wana hasiri kwa sababu wanaamini Gunners wanafanya kusudi ili kumvuruga akili mchezaji huyo. (Mirror)
REUTERS
Atletico Madrid wanataka kumsajili Lacazette kuchukua nafasi ya mshambuliaji Antoine Griezmann, 28 ambaye anaelekea Barcelona. (Mirror)
Winga wa Barcelona na Ufaransa Ousmane Dembele, 22, hana mpango wa kuondoka Nou Camp msimu huu wa joto licha ya vilabu vikubwa Ulaya ikiwa ni pamoja na Liverpool na Bayern Munich kuonesha nia ya kutaka kumsajili. (L'Equipe)
Barcelona wako tayari kupokea maombi ya kumnunua mlinzi wa kati wa miaka 25-Mfaransa Samuel Umtiti, ambaye analengwa na Manchester United. (Sport, via Mirror)
GETTY IMAGES
Chelsea wameafikiana kuhusu mkataba mpya wa muda mrefu na kiungo wa kati wa England Ruben Loftus-Cheek, 23. (Telegraph)
Mlizi wa Arsenal Mfaransa Laurent Koscielny, 33,ananyatiwa na Bordeaux. (L'Equipe)
Tetesi Bora Jumanne
Kiungo wa kati wa Ufaransa Paul Pogba, 26, amekuwa akifanya mazoezi mjini New York licha ya wachezaji wenzake kurejea kambini kwa mazoezi ya kabla ya msimu mpya kuanza. (Sun)
GETTY IMAGES
Barcelona wako tayari kulipa euro milioni 100 ya kumwezesha mshambuliaji wa Inter Milan Muargentina Lautaro Martinez, 21 kuondoka klabu hiyo kabla mkataba wake kukamilika. (Corriere dello Sport - in Italian)
Winga wa Manchester City Mjerumani Leroy Sane ameangaziwa katika uzinduzi wa jezi za msimu wa mwaka 2019-20, licha ya tetesi kuwa Bayern Munich wamekuwa wakimnyatia nyota huyo wa miaka 23. (Express)
GETTY IMAGES

No comments:
Post a Comment