We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Monday, July 29, 2019

Simba yaja na 'Iga Ufe'

Klabu ya Soka ya Simba, imezindua wiki maalum ya kuelekea tamasha lake la siku ya Simba (Simba Day), litakalofanyika Agosti 6, 2019, ambapo kwa mwaka huu wamekuja na kauli mbiu inayosema 'Iga Ufe, This Is Next Level'.

Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es salaam, Msemaji wa Klabu ya Simba, Haji Manara amesema kwa mwaka huu tamasha hilo litakuwa la aina yake.
"Tukio letu la wiki ya Simba limeigwa maeneo mbalimbali, lakini sisi tutataka kulifanya kwa ubora zaidi, na kauli mbiu yetu itaitwa 'Iga Ufe, This is Next Level #10 Years Anniversary Of Simba Wiki" amesema Manara.
Awali Mtendaji Mkuu wa Simba Crescentius Magori, amesema wiki ya Simba imetawaliwa na matukio mbalimbali ikiwemo utoaji damu, pamoja kutoa misaada kwenye Hospitali mbalimbali nchini.
"Tarehe 3 Agosti, nchi nzima iwe nyekundu, twende kwenye Mahospitali tukawasaidie watu wasiokuwa na uwezo. Mungu ametujaalia mwaka jana tumefanya vizuri sana inabidi mwaka huu tupate baraka za watu hawa wenye uhitaji." amesema Magori.

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list