Msafara wa kikosi cha Simba unaondoka Afrika Kusini leo kurejea nchini baada ya kumaliza kambi ya wiki mbili
Mabingwa hao wa nchini wanarudi kumalizia maandalizi nyumbani tayari kwa Tamasha la Simba Day litakalofanyika Jumanne ijayo, August 06 kwenye uwanja wa Taifa
Siku hiyo Simba itatambulisha kikosi chake kwa kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Power Dynamo ya Zambia
Baadae Simba itaelekea nchini Msumbiji kuikabili UD Songo kwenye mchezo wa kwanza wa ligi ya mabingwa hatua ya awali, August 10
Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems ameeleza kuridhishwa na kambi waliyoweka Afrika Kusini ambapo amesema wachezaji wake wameiva tayari kwa mikiki mikiki ya msimu mpya
No comments:
Post a Comment