Mafanikio iliyopata Simba msimu uliopita yameisaidia timu hiyo kujihakikishia nafasi ya kuanzia raundi ya kwanza michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika
Kama itafanikiwa kuvuka hatua hiyo, moja kwa moja Simba itatinga hatua ya makundi
Na hata kama ikitolewa, itacheza raundi ya pili ya michuano ya kombe la Shirikisho
Simba ilifanikiwa kutinga robo fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa msimu uliopita na kujivunia alama 15
Alama hizo zimesaidia kuongezwa kwa idadi ya timu za Tanzania zitakazoshiriki michuano ya CAF msimu ujao
Yanga itashiriki michuano ya ligi ya mabingwa sambamba na Simba lakini yenyewe itaanzia hatua ya awali
Azam Fc na KMC nazo zitashiriki kombe la Shirikisho zikitarajiwa kuanzia hatua ya awali pia

No comments:
Post a Comment