Uongozi wa Yanga umeshamalizana na Bandari Fc kuhusu usajili wa mlinda lango Farouq Shikalo ambaye sasa atajiunga na Yanga baada ya michuano ya Kagame kumalizika nchini Rwanda
Kocha Mkuu wa Bandari Fc Benard Mwalala ambaye ni mshambuliaji wa zamani wa Yanga, amethibitisha kuwa Shikalo atajiunga na Yanga baada ya michuano hiyo kumalizika
"Farouq atajiunga na Yanga baada ya michuano ya Kagame kumalizika, ni baada ya makubaliano kufikiwa"
"Klabu ya Bandari Fc inamtakia kila la kheri," imesema taarifa ya Mwalala
Yanga tayari imeanza mazoezi mkoani Morogoro kujiandaa na msimu mpya wa ligi kuu ya Tanzania Bara na michuano mbalimbali

No comments:
Post a Comment