Serikali ya Kenya ipo kwenye mchakato wa kutaifisha shirika lake la Ndege la Kenya Airways (KQ), Hii ni baada ya shirika hilo kuingiza hasara kwa miaka minne mfululizo.
Mchakato wa kulitaifisha shirika la ndege la Kenya airways (KQ), umeanza rasmi, baada ya bunge la nchi hiyo kupitisha kwa pamoja ripoti ya kamati ya uchukuzi inayotaka serikali kusimamia shirika hilo.
Kupitishwa kwa ripoti hiyo kuna maana kwamba serikali ya Kenya italazimika kulipa madeni yote ya shirika la ndege la Kenya airways kabla ya kutaifishwa.
Selikali ya Kenya inayomiliki hisa asilimia 48.9, Imechukua hatua ya kulitaifisha shirika la ndege la Kenya airways, ili kulinusuru na madeni yanayoendelea kuongezeka.
Shirika la KLM, linamiliki asilimia 7.8 ya hisa za shirika hilo la ndege. Asilimia 38.1 ya hisa inamilikiwa na kampuni zinazoikopesha Kenya airways.
Katika juhudi za kulinusuru shiika hilo, Kenya Airways ilipendekeza kusimamia uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta kwa muda wa miaka 30, ili kuimarisha mapato yake, baada ya kupata hasara ya dola bilioni 2 mwaka 2017, mpango uliokataliwa na kamati ya bunge kuhusu uchukuzi.
Kamati ya bunge badala yake ilipendekeza kwamba shirika hilo litaifishwe, katika ripoti iliyowasilishwa bungeni Juni 18 mwaka huu.
Hata hivyo, Wabunge wa Kenya wametofautiana kuhusu jinsi ya kulipa madeni ya KQ, baadhi wakisema wananchi walipa kodi hawastahili kugharamia makosa ya usimamizi yaliyofanywa na watu binafsi, na kutaka wamiliki wa sasa wa hisa za shirika hilo kugharamia hasara. Baadaye wamekubaliana kwamba serikali itabeba mzigo wa kulipa madeni yote.
No comments:
Post a Comment