Mkutano Mkuu wa 35 ALAT Taifa unaendelea jijini Mwanza huku Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa akitarajiwa kuuzindua rasmi baadaye ukiwa ni mkutano wa siku tatu ulioanza jana Jumatatu, Julai 22.
Katika salaam za awali za Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Magu ambaye pia ni Mwenyekiti wa ALAT Mkoa wa Mwanza, Hilali Elisha amemuomba waziri mkuu kuangalia upya waraka uliopunguza posho za madiwani.
Amesema kuwa katika waraka huo yalitolewa maelekezo ya kupunguzwa kwa posho hizo hadi kufikia Shilingi 40,000 kwa kikao na kufuta malipo ya nauli za madiwani kitendo kilichowafanya madiwani hao kuishi kwa shida na kupunguza kasi ya kuwaletea maendeleo wananchi.
No comments:
Post a Comment