Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Ally Hapi amesema kuwa katika viongozi wote wa Awamu ya Nne, Bernald Membe ni kiongozi muongo kuliko wote.
Hapi amesema hayo leo Mkoani humo katika Mkutano wake na Waandishi wa habari ameomba kumkumbusha Membe kuwa Rais anawekwa na Mungu "Sisi vijana hatutasita kuwakabili kama mbwai na iwe mbwai kwasababu nchi hii sisi tutabaki nayo kuliko wazee ambao muda wao umekwisha."
"Membe ana usafi gani , Waziri aliyekuwa muongo katika Mawaziri wote wa Awamu ya Nne, hakuna mtu muongo kama Membe katika nchi hii aliwadanganya viongozi wenzie kipindi cha Kikwete kuwa ndi next President , Rais anawekwa na Mungu," amesema leo Hapi.
"Nakuomba Mh. Rais kazi ya kupambana na kutulinda tuachie sisi , kazi ya kushughulika na watu kama wakina Membe tuachie sisi kwanza tunawajua, tunataka Rais wetu aendelee kukaa kwenye focus ya nchi yetu," alisema Hapi.
No comments:
Post a Comment