Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems amekiri kuwa kuondoka kwa kiungo James Kotei na mshambuliaji Emmanuel Okwi ilikuwa ni 'sapraizi' kwake lakini anaheshimu uamuzi wao
Aussems ambaye yuko Afika Kusini akikinoa kikosi cha Simba tayari kwa msimu mpya, amesema wachezaji hao walikuwa katika mipango yake ya msimu ujao
Hata hivyo asingeweza kuwazuia kwa kuwa walipata timu zilizowapa maslahi makubwa zaidi
"Okwi na Kotei ni miongoni mwa wachezaji ambao nilipendekeza tuendelee kubaki nao, lakini mwisho wa siku mchezaji mwenyewe ndio mwenye uamuzi wa mwisho," alisema
"Walinitaarifu kuwa wamepata timu zitakazowapa maslahi zaidi hivyo mimi niliwatakia kila la kheri japo nilipenda tuendelee kuwa nao"
Kotei amesajiliwa na klabu ya Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini wakati Okwi anaelekea Falme za kiarabu
Simba imemsajili kiungo Sharaff Shiboub kutoka El Hilal ya Sudan kuchukua nafasi ya Kotei wakati nafasi ya Okwi itazibwa na nyota wa kigeni ambaye uongozi uliahidi utamsajili karibuni
No comments:
Post a Comment