We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Monday, July 22, 2019

Kubenea aitaja TCRA, sakata la Nape na Kinana

Mbunge wa Ubungo kupitia (CHADEMA) Saed Kubenea, ameiomba Mamlaka ya Mawasiliano Nchini (TCRA), itoe taarifa sahihi juu ya nani aliyefanyakazi ya kusambaza sauti mbalimbali katika mitandao ya kijamii hivi karibuni zikisikika sauti zinadhaniwa kuwa ni za Nape akizungumza na Kinana.

Hayo ameyabainisha leo Julai 22, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar Es Salaam.
Kubenea amesema kuwa lazima faragha za watu ziheshimiwe, kwa sababu nchi hii inawatu wengi wakiwemo mabalozi wanaowakilisha nchi mbalimbali hali anayodai huenda ikaweza kuiingiza TCRA katika mgogoro wa kufungiwa na shirika la mawasiliano la kimataifa.
''TCRA itoe taarifa sahihi juu ya nani aliyefanya kazi hiyo, kama Kinana na Nape amerekodiwa nani ana uhakika kama balozi wa Marekani hajarekodiwa, balozi wa Uingereza hajarekodiwa, viongozi wetu wa vyombo vikubwa hawajarekodiwa, kama wamerekodiana wenyewe kwa wenyewe sisi vipi, wengine vipi, tuache huu utamaduni'' amesema Kubenea.
Aidha Kubenea ameongeza kuwa, kuna baadhi ya sauti zinazosadikikia ni za Makamba akiongea na January, hivyo TCRA inalojambo la kueleza ni nani anayefanyakazi ya kuwarekodi na hofu yake ni kwamba watu hawa wameanza kufuatiliwa muda mrefu, na vipi zikivuja sauti zinazoonyesha wanaongea na nyumba ndogo, inaweza kuleta mtafaruku katika familia zao.
''Wale wanaorekodi hawaedit, wanaedit wanavovitaka wao  pengine kuna mengine mazuri tu yakutaka kumshauri Rais, kama wanataka basi waachie vyote tusikilize siku nzima, watu wanafaragha na ni lazima faragha zilindwe sio vitu vinatolewa tu part 1, 2,3,5 imekuwa kama movie sasa''. amesema Kubenea.

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list