We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Thursday, July 4, 2019

RC awataka wananchi kujitokeza kumpokea Rais Kenyatta


Mkuu wa mkoa wa Geita (RC) nchini Tanzania, Robert Gabriel amewataka wananchi mkoani humo kujitokeza kwa wingi kumpokea Rais wa Kenya, Uhuru Kenyata anayetarajiwa kuwasilia Uwanja wa Ndege Chato kesho Ijumaa Julai 5, 2019.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jioni Jumatano Julai 3, 2019, Gabriel alisema ni fursa kwa wakazi wa Geita kuonyesha uzalendo na kushiriki kumpokea Rais Kenyatta ambaye anatua kwenye Uwanja wa Chato kwa mara ya kwanza.
Gabriel aliwataka wananchi kukaa kwenye viunga vya barabara kuanzia eneo la uwanja wa ndege hadi kijiji cha Mlimani kuanzia saa 12 asubuhi kwa lengo la kumpokea kiongozi huyo.
Alisema ujio huo ni fursa kwa mkoa wa Geita kuendelea kutambulika kitaifa na kutaka wananchi kuchangamkia fursa za kibiashara katika soko wala Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Taarifa iliyotolewa jana Jumatano na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu ya Tanzania, ilisema Rais Kenyatta atawasili nchini kwa ziara binafsi ya siku mbili kwa mwaliko wa Rais wa Tanzania, John Magufuli.


Taarifa hiyo ilisema Rais Kenyatta atawasili katika uwanja huo saa 4 asubuhi kisha atakwenda nyumbani kwa Rais Magufuli katika Kijiji cha Mlimani, Chato ambako atafanya mazungumzo na Jumamosi ya Julai 6, 2019 Rais Kenyatta ataondoka.

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list