We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Thursday, July 25, 2019

Rais wa Tunisia afariki dunia


Rais wa Tunisia Beji Caid Essebsi amefariki dunia akiwa na miaka 92.
Essebsi ambaye anaminika kuwa ndiyo Rais mkongwe zaidi duniani amefariki leo Alhamisi Julai 25, katika Hospitali ya Jeshi la Tunisia alipolazwa kwa ajili ya matibabu.
Hata hivyo, haikuelezwa wazi Rais huyo alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa gani.
Mwezi uliyopita hali ya Rais Essebsi ilianza kutetereka na kulazwa kwa muda katika hospitali hiyo.
Rais Essebsi aliingia madarakani baada ya kushinda uchaguzi huru wa kwanza wa nchi hiyo kufuatia vuguvugu la maandamano katika mataifa ya kiarabu.
Tume ya Uchaguzi nchini Tunisia ilimtangaza Essebsi baada ya kumshinda Rais aliyekuwa madarakani, Moncef Marzouk.
Kuchaguliwa kwa Rais Essebsi kulihitimisha mvutano wa demokrasia wa miaka minne ya ghasia zilizoghubika Taifa hilo zilizosababisha kung'olewa kwa utawala wa Rais Zine el-Abedine Ben Ali.

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list