Rais wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amesema kuwa ataandika barua rasmi ya Pongezi kwa Askari wa Kenya na kwenda kwa vyombo vya Ulinzi na Usalama wa Kenya.
Rais Magufuli amesema sababu za kuandika barua hiyo kwa Askari ni kutoa pongezi za kusaidia kukamatwa kwa mali za Watanzani ambayo ni dhahabu.
"Nitaandika Barua rasmi ya Pongezi kwa Askari wa Kenya kwenda kwa vyombo vya Ulinzi na Usalama wa Kenya kwa kusaidia kukamatwa kwa hizi mali za Watanzania, nitaangalia kwa namna gani siku za mbeleni tutawapongeza kwa kuwapa zawadi waliofanikisha kukamatwa kwa dhahabu yetu, ” amesema Rais Magufuli.
Rais Magufuli ameyasema hayo katika hafla ya makabidhiano ya dhahabu iliyokamatwa nchini Kenya iliyowasilishwa na Mjumbe Maalum wa Rais wa Kenya, Kenyatta leo Julai 24, 2019. Ambapo hafla ya makabidhiano hayo imefanyika Ikulu Jijini Dar.
No comments:
Post a Comment