Staa wa Liverpool na timu ya taifa ya Misri, Mohamed Salah ametembelea nchini Kenya Jumanne, ambapo alitembelea katika maeneo ambayo hayakuweza kufahamika.
Inaelezwa kuwa alilala katika hoteli ya Hilton Garden Inn inayopatikana barabara ya Mombasa Jijini Nairobi, na kwa mujibu wa wahudumu wa hoteli hiyo, Mo Salah ameondoka asubuhi ya leo Jumatano akiwa na ulinzi mkali.
"Timu ya watu wake wa karibu ilikuja hapa na kuongea na mmoja wa mabosi wetu, hawakutaka taarifa yoyote itolewe ingawa tulifurahia uwepo wake", amesema mmoja wa wahudumu wa hoteli hiyo, akiuambia mtandao wa Star.
Pia inaelezwa kuwa staa huyo amelala chumba chenye gharama ya Sh 30,000 za Kenya ambazo ni sawa na Sh. 662,757.16 za Kitanzania.
"Hatukujua ni wapi alikuwa anakwenda", amesema mhudumu wa pili ambaye alizungumzia suala hilo.
Mohamed Salah yuko likizo hivi sasa baada ya kutoka katika michuano ya mataifa ya Afrika, ambapo timu ya taifa ya Misri ilitolewa katika hatua ya 16 bora na Afrika Kusini.
No comments:
Post a Comment