Ziara hiyo ya Mbowe ambaye ni Mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani Tanzania cha Chadema ilitakiwa ianze leo lakini iliahirishwa jana Jumapili Julia 28, 2019 baada ya mbunge huyo kufiwa na kaka yake, Meja Jenerali Alfredy Mbowe.
Leo Jumatatu Julai 29, 2019 barua iliyotolewa na Mkuu wa Polisi wilayani ya Hai, Lwelwe Mpina yenye kumbukumbu namba MB/JH/27/07/2019 kwenda kwa katibu wa mbunge (Mbowe) imezungumzia kusitishwa kwa ziara hizo za Mbowe.
Aidha barua hiyo ilieleza sababu za kusitishwa kwa ziara ya Mbowe ni kutokana na Mkuu wa Wilaya hiyo, Lengai Ole Sabaya kuwa na ziara ya kukagua miradi ya maendeleo na kusikiliza kero mbalimbali za wananchi hivyo kuingiliana kwa mikutano hiyo kungeweza kusababisha uvunjifu wa amani kutokana na ufinyu wa nguvu kazi.
“Kwa busara, sitisha ziara na mikutano unayotegemea kuifanya hadi mkuu wa wilaya atakapomaliza ziara yake,” inasomeka barua hiyo
Mwananchi ilipozungumza na Mkuu wa Wilaya hiyo (DC), Ole Sabaya ambaye amekiri kuwepo kwa ziara zake zilizoanza Julai 24, 2019 za kukagua miradi ya maendeleo na kusikiliza kero mbalimbali za wananchi.
No comments:
Post a Comment