We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Monday, July 8, 2019

PICHA: Hawa ndio wafanyakazi Azam TV waliofariki dunia ajalini



Wafanyakazi watano wa kampuni ya Azam Media wamefariki dunia leo Jumatatu Julai 8, 2019 katika ajali ya gari iliyotokea eneo la Shelui mkoani Singida baada ya gari aina ya Coaster walilokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso la lori.

Mkurugenzi wa uzalishaji vipindi wa kampuni hiyo, Yahya Mohamed amewataja waliofariki dunia kuwa ni Salim Mhando, Florence Ndibalema, Said Haji, Sylvanus Kasongo na Charles Wandwi.
Mbali na wafanyakazi hao, watu wengine wawili wamefariki dunia katika ajali hiyo ambao ni madereva wa Coaster lililokuwa limewapakia wafanyakazi 10 wa kampuni hiyo, pamoja na dereva wa lori.
Wafanyakazi hao walikuwa wakielekea wilayani Chato Mkoa wa Geita katika uzinduzi wa Hifadhi ya Taifa ya Chato-Burigi.
Uzinduzi wa Hifadhi hiyo unafanyika kesho Jumanne Julai 9, 2019 na Rais wa Tanzania, John Magufuli.



No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list