Mshambuliaji wa Kimataifa wa Uganda Emmanuel Okwi ametimkia Falme za Kiarabu ambapo amesajiliwa na Fujairah Fc inayoshiriki ligi kuu nchini humo
Licha ya kuondoka Simba, Okwi amewataka wachezaji wa timu hiyo walinde mafanikio yaliyopatikana msimu uliopita na pengine wavuke zaidi
Katika misimu miwili aliyocheza Simba, Okwi aliisaidia Simba kutwaa mataji mawili ya ligi kuu pamoja na kufika robo fainali michuano ya ligi ya mabingwa msimu uliopita
Mshambuliaji huyo amewaaga wachezaji wenzake kupitia ukurasa wao wa mtandao wa WhatsApp
Okwi amesema amejiunga na timu hiyo ya Arabuni kutokana na maslahi makubwa waliyompa

No comments:
Post a Comment