Wachezaji wa kigeni waliosajiliwa na Simba kwa ajili ya msimu ujao, wanatarajiwa kuanza kuwasili leo Ijumaa tayari kuelekea kambini kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya
Kocha Mkuu wa mabingwa hao wa Tanzania Bara mara mbili mfululizo Patrick Aussems alitarajiwa kuwasili nchini jana
Simba inatarajiwa kuondoka mwishoni mwa wiki kuelekea Afrika Kusini ambako itaweka kambi
Msemaji wa Simba Haji Manara amesema maandalizi ya kambi hiyo yako tayari na mpaka kufikia Jumatatu, timu itakuwa imeondoka Dar
Kikosi cha simba kilichosajiliwa msimu huu ni pamoja na Kagere, Shiboub, Francis Kahata, Tairone santos da silva, Person Fraga Viera, Wilker Henrique da silva, Deo Kanda, Ibrahim Ajibu, Beno Kakolanya na Kennedy Juma.
Wachezaji wengine ni John Bocco, Pascal Wawa, shomari Kapombe, Erasto Nyoni, Aishi Manula, Clatous Chama, Jonas Mkude, Rashid Juma, Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ Hassan Dilunga, Said Ndemla na Mzamiru Yassin

No comments:
Post a Comment