Ninja amekiri kamati ya usajili ya Yanga, imefanya kazi nzuri ya kushusha majembe ya maana kwa ajili ya msimu ujao, lakini neno moja kwa viongozi wa klabu hiyo aliwataka watengeneze umoja.
Anafafanua umoja unaohitajika Yanga kwamba ni viongozi kuwa karibu na wachezaji wote bila kujali majina yao na kwamba ndipo lengo wanalolitarajia kwa msimu ujao litatimia.
"Simba na Yanga zinapaswa kujua kwamba usajili peke yake haitoshi, zinapofanya kazi na mchezaji lazima ziwe na upendo wa kuwajenga saikolojia zao, hata wanapopata matatizo wafanye walezi wema.
"Nje ya umoja na mshikamano hata angeletwa Cristiano Ronaldo itakuwa kazi bure, jambo la msingi ninaloweza kuwashauri viongozi wa Yanga ni kwamba penye upendo kuna mafanikio ya hali ya juu.
"Asilimia kubwa ya wachezaji waliosajiliwa ni wazuri, ila wajue namna ya kuishi nao ili waweze kufikia lengo la kuchukua ubingwa msimu ujao, wote wawachukulie hali moja sio kubagua kuwaona wengine wa hali ya chini,"anasema.
Ninja alisajiliwa na Yanga akitokea Taifa Jang'ombe ya Zanzibar, ameichezea klabu hiyo kwa misimu miwili na alikuwa mchezaji muhimu kwenye kikosi cha kwanza cha kocha Mwinyi Zahera na sasa atakuwa anasikika anga za nje.

No comments:
Post a Comment