Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Prof.Joyce Ndalichako, amegiza kuondolewa katika nafasi zao Afisa Mdhibiti Ubora wa Elimu Kanda ya Magharibi, Khalid Nuru, Afisa Mdhibiti Ubora Msaidizi Paul Bigashi na Afisa Mdhibiti Ubora wa Manispaa ya Kigoma Ujiji, kwa kukaidi maagizo ya mamlaka.
July 18 mwaka huu Prof. Ndalichako,alitembelea na kukagua ujenzi wa ofisi za udhibiti ubora wa elimu katika Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma na Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji ambapo aliagiza kubomolewa na kurekebishwa baada ya kutoridhishwa na vipimo vya saruji vilivyotumika katika hatua ya sakafu ya ujenzi huo.
Hata hivyo katika ziara yake ya ghafla aliyoifanya leo amebaini maelekezo yake kutotekelezwa na kumuagiza Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, kuwaondoa wadhibiti ubora hao na kuwapangia kazi nyingine.
No comments:
Post a Comment