Akizungumza leo Jumatatu Julai 8 2019, Mkurugenzi wa Takwimu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Daniel Masolwa amesema hiyo inamaanisha kuwa kasi ya mabadiliko ya bei ya bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia Juni 2019 imeongezeka ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia Mei 2019.
Amesema kuongezeka kwa mfumuko wa bei wa Taifa kwa mwaka ulioishia Juni 2019 kumechangiwa na bei za bidhaa za vyakula na zisizokuwa za vyakula katika kipindi cha mwaka unaoishia Juni 2019

No comments:
Post a Comment