Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhandisi Hamadi Masauni, amefika katika kijiji cha Kihamba, halmashauri ya mji wa Nanyamba mkoani Mtwara na kuzungumza na wananchi waliopoteza ndugu zao kwa kupigwa Risasi na watu ambao hawajafahamika katika kijiji cha Mtole nchini Msumbiji.
Katika maelezo yake, Naibu waziri Masauni amewahikiiishia wananchi hao kuimarishwa kwa hali ya usalama katika maeneo hayo ya Mipakani pamoja na kuahidi kuwasaka na kuwakamata Wauaji hao waliowapiga Risasi na kuwaua Watanzania Kumi katika tukio la Juni 26 mwaka huu.


No comments:
Post a Comment