Jina la kiungo Mohammed Inrahim 'Mo' halimo kwenye orodha ya kikosi cha Simba kwa ajili ya msimu ujao
Wengi wamejiuliza kama kiungo huyo ameachwa au la?
Ukweli ni kwamba Mo bado ni mchezaji wa Simba lakini ametolewa kwa mkopo kwenda klabu ya KMC
Mo bado ana mkataba wa mwaka mmoja na Simba
Lakini huenda akaondoka moja kwa moja baada ya mkataba wake kumalizika
Simba imemsajili winga Miraji Athumani ambaye ametajwa kuchukua nafasi ya Mo
Mchezaji mwingine aliyetolewa kwa mkopo ni mshambuliaji Adam Salamba

No comments:
Post a Comment