Mchezo wa kwanza wa kusaka nafasi ya kutinga fainali za CHAN 2020 kwa wachezaji wanaocheza ndani kati ya Tanzania dhidi ya Kenya umemalizika kwa suluhu ya bila kufungana
Licha ya kutawala mchezo huo kwa muda mrefu, Stars ilikosa mbinu ya kuipenya ngome ya Kenya
Ulikuwa ni mchezo ambao Kenya walionekana kucheza kwa kujihami zaidi wakitafuta matokeo ya sare, wakati Stars ilishambulia sana lango lao lakini umaliziaji ulikuwa tatizo
Matokeo hayo yameiweka mtegoni Stars kwani inapaswa kushinda ugenini ili kuweza kusonga mbele hatua inayofuata
Mchezo wa marudiano utapigwa August 04 kwenye uwanja wa Kasarani nchini Kenya

No comments:
Post a Comment