Uongozi wa Yanga umeamua kulifanyia maboresho benchi lake la ufundi upande wa kocha wa makipa ambapo mlinda lango wa zamani wa timu hiyo Peter Manyika anatajwa kuchukua nafasi ya Juma Pondamali
Awali Yanga ilimuhitaji Razak Ssiwa kutoka Bandari Fc ya Kenya
Hata hivyo inaelezwa kumekuwa na ugumu kumpata mlinda lango huyo ambaye alikuwa akihusishwa kutua Yanga tangu msimu uliopita
Pondamali amekuwa kocha wa makipa wa Yanga kwa zaidi ya misimu minne
Manyika atakuwa na kazi ya kuhakikisha viwango vya walinda lango wa Yanga Farouq Shikalo, Metacha Mnata na Klaus Kindoki vinakuwa kwenye ubora wakati wote

No comments:
Post a Comment