Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda amepinga uamuzi wa wachezaji Kelvin Yondani na Erasto Nyoni kustaafu kuitumikia timu ya Taifa
Wachezaji hao walitangaza kustaafu kuichezea Stars muda mfupi baada ya Stars kuondoshwa michuano ya Afcon 2019 hatua ya makundi
Hata hivyo baada ya Stars kurejea nchini jana, Makonda alipinga hatua hiyo na kuwataka waendelee kulitumikia Taifa
Wachezaji hao wamekubali kuendelea kuichezea Stars
Yondani na Nyoni ndio wachezaji waliocheza timu ya Taifa kwa muda mrefu, wakiitumikia timu hiyo kwa zaidi ya miaka 11

No comments:
Post a Comment