We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Sunday, July 7, 2019

Lugola aruhusu mabasi kusafiri saa 24 nchini Tanzania


Waziri wa Mambo ya Ndani nchini Tanzania, Kangi Lugola amepiga marufuku makamanda wa polisi wa mikoa nchini kuzuia mabasi yanayofanya safari katika ya Jiji la Dar es Salaam na Mikoa ya Kanda ya ziwa kusafiri usiku kwa kisingizio cha kuhofia kuvamiwa na majambazi.

Ametoa kauli hiyo leo Jumapili Julai 7, 2019 katika mkutano wa hadhara uliohudhuriwa na wananchi wa vijiji vya Namibu na Mwibara wilayani Bunda mkoani Mara.
Taarifa iliyotolewa na wizara hiyo imemnukuu mbunge huyo wa Mwibara (CCM) akisisitiza kuwa mabasi yanayotoka mikoa ya Kanda ya ziwa kwenda Dar es Salaam kutuzuiwa mkoani Morogoro na yanayotoka Dar es Salaam kwenda katika mikoa hiyo kutozuiwa yanapofika mkoani Shinyanga.
“Hatuwezi kupangiwa ratiba ya kusafiri na majambazi, Serikali ipo imara pamoja na polisi. Niliwahi kutoa agizo majambazi wote wasambaratishwe, asakwe hadi jambazi wa mwisho na  akamatwe kama kuku.”
“Taarifa za uhalifu zinaonyesha polisi imefanya kazi kubwa kupambana na uhalifu na hasa majambazi, niliwahi kusema  kipindi hiki si cha huruma na majambazi bali cha kuhakikisha wananchi wanaishi kwa amani,” amesema Lugola.

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list